Home �
News de stars
� UPDATE:PICHA ZA MAPOKEZI YA AZONTO AHAIDI KUFANYA MAKUBWA NDANI YA JIJI.
Mac For Worlding |
7.9.13 |
0
commentaires
Mwanamuziki ODG Maarufu kwa jina la Azonto akiwa ndani ya ulinzi mkali
Azonto
kulia akiwa na na baunsa wake huku msanii wa Bongo Movie Manaiki Sanga
"the don" akitoa maelekezo kwa mwanamuziki huyo ndani ya Hotel ya JB
BELMOND alipofikia mwanamuziki huyo
Msanii
wa
Bongo Muvie Prince Kas ambae yuko kwenye kamati ya mapokezi ya
mwanamuziki huyo asubuhi ya leo kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa
Da'salam
Manaiki Sanga "The Don" naye yuko kwenye kamati ya ujio wa mwanamuziki Azonto akiwakaribisha wageni hao
Msanii Fuse ODG (wa pili kulia) akiserebuka ngoma yake ya Azonto pamoja na waandishi wa habari.
Fuse
ODG akizungumza na waandishi wa habari, (hawapo pichani) na kulia ni
Afisa Biashara Mkuu wa Zantel, Sajid Khan na kushoto ni Mkurugenzi wa
Radio ya Times FM, Rehure Nyaulawa.
Fuse ODG akipozi na wanahabari.
Fuse ODG akitoka katika Hoteli ya Kilimanjaro baada ya mkutano wake na waandishi.
Mwanamuziki mahiri kutoka nchini Ghana, Fuse ODG, aliyewasili leo
jijini Dar es Salaam, ameahidi kufanya makamuzi ya kufa mtu kesho.
Akizungumza
kwenye mkutano na Waandishi wa habari uliofanyika katika Hoteli ya
Kilimanjaro, Posta alasiri leo, Fuse alisema amefurahi kufika Tanzania
na kuwaahidi wapenzi wa burudani hususan wa nyimbo zake ukiwano wa
Azonto kuwa watapata kile kitu roho inapenda.
Afisa Biashara Mkuu wa
Zantel, Sajid Khan aliyeongozana na mwanamuziki huyo kwenye mkutano huo
wa Waandishi wa Habari alisema Zantel imemleta mwanamuziki huyo ili
kuwapa ari wasanii wa ndani wenye lengo la kufikisha kazi zao hatua ya
kimataifa.
“Zantel imekuwa mstari wa mbele katika kuwawezesha wasanii
wa ndani, hasa vijana, na kwa kumleta Fuse ODG, ambaye ni mmoja wa
wasanii wachache kutoka Afrika waliofanikiwa kufikisha muziki wao soko
la kimataifa, tunaamini vijana watajifunza mengi,” alisema Khan.
Naye
Mkurugenzi Mtendaji wa Radio Times FM, Rehure Nyaulawa alisema
wamemleta msanii huyo ili kuhakikisha Watanzania wanapata burudani
wanayoipenda ya Azonto hapa nchini.
“Azonto imejipatia umaarufu
mkubwa karibu dunia nzima, lakini pia kwa upande wa radio yetu wimbo huu
umepata maombi mengi kuliko wimbo wowote wa kimataifa kiasi cha kuona
tuwaletee Watanzania burudani wanayoipenda,” alisema Nyaulawa.
Shoo
ya mwanamuziki huyo itafanyika kesho katika Viwanja vya Chuo cha Ustawi
wa Jamii Kijitonyama na burudani itaanza saa mbili usiku hadi majogoo.
Kiingilio katika shoo hiyo kitakuwa shilingi 10,000 kwa kununua tiketi kabla na shilingi 15,000 kwa kununua mlangoni.
Msanii kutoka nchini Ghana Fuse ODG anaetamba na ngoma zake kama
vile Azonto na Antenna tayari ameshatua katika ardhi ya Tazania.
Wasanii wa Bongo watakao washa moto ni Dogo Janja, Wakazi,Snura, H.Baba, Madee na wengine kibao watakuepo.
Category:
News de stars
About GalleryBloggerTemplates.com:
GalleryBloggerTemplates.com is Free Blogger Templates Gallery. We provide Blogger templates for free. You can find about tutorials, blogger hacks, SEO optimization, tips and tricks here!