DULLY SYKES "NAMFANANISHA DIAMOND NA MAREHEMU KANUMBA KWA UWEZO WA KUTHUBUTU"
Dully Sykes alikuwa akiongea na Bongo5 kwenye uzinduzi wa video ya video mpya ya Diamond uliofanyika wiki iliyopita kwenye ukumbi wa Serena Hotel jijini Dar es Salaam.
“Diamond ni namba moja kwasababu yupo tayari kujitoka kwa kila kitu,” alisema Dully. “Naweza kumfananisha Diamond na mtu kama Kanumba. Kanumba alikuwa ana uwezo wa hata kuchukua nauli yake ya kwenda sehemu kama Ghana kwenye tamasha la movie lakini ilimradi kujitengenezea status yake. Kwahiyo Diamond ni mtu ambaye tayari ameshajitolea kwaajili ya kuutetea muziki wetu.”
Pia Dully amesema mwishoni mwa mwaka huu anatarajia kuiongezea vifaa vipya studio yake ‘4.12’ ili kujiimarisha zaidi kwenye utayarishaji wa muziki ambao anasema kwa sasa anaufurahia zaidi kuliko hata kuimba.
Category: News de stars
0 commentaires