UZINDUZI WA FOOLISH AGE WAFUNIKA MASTAR KIBAO WAHUDHURI, LULU ATUZWA PESA KIBAO.
Mac For Worlding |
31.8.13 |
0
commentaires
UZINDUZI WA FOOLISH AGE WAFUNIKA MASTAR KIBAO WAHUDHURI, LULU ATUZWA PESA KIBAO.
UIMBAJI stadi wa Wimbo wa YAHAYA wa Nguli wa muziki wa Kizaki
kipya Lady Jay Dee umemjaza mahela Msanii wa Filamu aliyejizolea umaarufu kwa
miaka ya hivi karibuni, Elizabeth Michael ‘Lulu’ wakati akiimba wimbo huo na
Jide wakati wa uzinduzi wa Video yake mpya na ya kwanza kusimama peke yake ya
FOOLISH AGE.
Baada ya movie hiyo kali ya dakika 120 iliyoonyesha ukali wa
staa huyo kuoneshwa kwa dakika 20 tu na kubakisha zingine 100 kusubiri wateja
kuziona majumbani kwao alipanda jukwaani kujitambulisha na kutoa shukrani kwa
wamepenzi wa tasnia ya filamu nchini Tanzania kwa muitikio wao alipanda na
kuimba wimbo huo wa Yahaya.
Akianzia kuimba kiitikio cha wimbo huo akiwa Back Stage,
Lulu aliwashangaza watu pale alipomudu vyema wimbo huo kiasi cha mashabiki ‘Mapedeshee’
wakiongozwa na Pedeshee Rich Rich, kupanda jukwaani na kumtunza fedha kibao
ambazo hakika zilimpagawisha msanii huyo na mwisho wa wimbo huo alisema mziki
unalipa.
“Jamanieee kumbe mziki unalipa ile mbaya yaani nimeimba ubeti mmoja tu hapa ona hela kibao,
kuanzia sasa na mimi nitaanza kuimba mziki”, alisikika Lulu akisenma huku
akishangiliwa na mashabiki wake.
Uzinduzi
wa fikamu hiyo ya kiswahili ambayo ina sub title ya Kiingereza na
ambayo haipaswi kuangaliwa na watoto chini ya miaka 16, huku ikiwa
imechezwa na wasanii maarufu na wakongwe kama Elizabeth Michael
mwenyewe, Diana Kimaro, Hashim Kambi, Ombeni Phiri na Mzee Jengua
ulifanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Wasanii mbalimbali walihudhuria show hiyo usiku huu pale Mlimani City
Lulu
akizungumza machache mara baada ya Move yake hiyo kuoneshwa kwa
mashabiki na wapenzi wa filamu Tanzania ndani ya Ukumbi wa Mlimani City.
Wadau walifuatilia burudani...
Jaydee akikamua jukwaani...
Mama na mwanae ni kama chanda na Pete... huyo ni Natasha (kulia) na Bintiye Monalisa.
.... Walitunzana tu kivyao vyao...
noti alizo tuzwa Jaydee...
Rich Rich akimwaga noti
Wadau wakifuatilia uzinduzi huo wa Filamu.
Furaha ilitawala
Mwogozaji wa Filamu za Swahiliwood, Leah Mwendamseke nae alikuwepo kuangalia kazi hiyo ya Lulu.
Waongoza Shughuli hiyo watangazaji wa Redio na TV Double G na mwana dada kutoka Times FM walikuwepo.
Category: News de stars
0 commentaires